[Verse 1]
Kichwa Wanipasua
Unanichapa Fimbo
Moyoni Napata Tabu,
Kichwa Wanipasua
Unanichapa Fimbo
Moyoni Napata Tabu,
Unajishaua
Una Maringo
Kama Una Sura Ya Dhahabu.
Una Maringo
Kama Una Sura Ya Dhahabu.
Ni Miaka Sasa Nakufata,
Ndara Zangu Zote Umekata,
Kutoka Tegeta Hadi Tabata,
Mpaka Visigino Vimechacha.
Ndara Zangu Zote Umekata,
Kutoka Tegeta Hadi Tabata,
Mpaka Visigino Vimechacha.
Mara Nasikia Kuna Bakari Kinyozi,
Ulishampa Hadi Kaka Yake Rose,
Kwani We Ni Pilipili Unitoe Machozi,
Nikikufata Waniletea Mapozi.
Ulishampa Hadi Kaka Yake Rose,
Kwani We Ni Pilipili Unitoe Machozi,
Nikikufata Waniletea Mapozi.
Mapenzi Uvumilivuu
Najua
Ila Kwako Nimeshindwa,
Upendo Sasa Majivuu
Umeungua
Basi Mama We Ndo Bingwa
[Chorus]
Ohh Mamy Looo (Sikupendi)
Utanitoa Rohoo (Sikupendi)
Kila Siku Jibu Lako Noo (Sikupendi)
Sikutamani Ng’o (Sikupendi)
Umeonyesha Dhahirii (Sikupendi)
Sikutamani Tena (Sikupendi)
Nimeghairi (Sikupendi)
Na Kwenu Siji Tena (Sikupendi).
[Verse 2]
Hadi Nahisi Na Gundu Mzee Mwenzenu
Kila Mambo Nikiset,
Nimegeuka Mlinzi Nyumbani Kwenu
Kila Siku Kwenye Geti.
Nilikufata Mpaka Kigogo,
Kwenye Shuhuri Yake Mama Asha Modo,
Ukanitukana Matusi Nina Shobo,
Pembeni Yuko Bwana Ako Bwebwe Chogo,
Akanitimba
Miguu Mikedekede,
Nikawa Mjinga
Tena Bwege Bwege,
Kama Nimetinga
Pombe MbegeMbege,
Alinishinda
Nikawa Legelege.
Nakata Tamaa Kuwa Nawe
Nikirudisha Kumbukumbu,
Nilipokuona Na Masawe
Kwenye Guest Ya Manungu,
Ulifanya Nipagawe
Kwa Mawazo Na Uchungu,
Nilikesha Nje Oh Mama Wee
Nikawa Chakula Cha Mbu.
[Bridge]
Mapenzi Uvumilivuu
Najua
Ila Kwako Nimeshindwa,
Upendo Sasa Majivuu
Umeungua
Basi Mama We Ndo Bingwa
[Chorus]
Ohh Mamy Looo (Sikupendi)
Utanitoa Rohoo (Sikupendi)
Kila Siku Jibu Lako Noo (Sikupendi)
Sikutamani Ng’o (Sikupendi)
Umeonyesha Dhahirii (Sikupendi)
Sikutamani Tena (Sikupendi)
Nimeghairi (Sikupendi)
Na Kwenu Siji Tena (Sikupendi) x2.
Sikutamani Tena (Sikupendi)
Nimeghairi (Sikupendi)
Na Kwenu Siji Tena (Sikupendi) x2.
My favorite
ReplyDelete